MKUTANO WA TANO WA KIKANDA AFRIKA KUHUSU HAKIMILIKI NA HAKISHIRIKI
Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kwa kushirikiana na shirika la kusimamia kazi za vielelezo vya kusikia na kuona (Global Audiovial Alliance-GAVA) na Shirika la Kikanda la Miliki Ubunifu Afrika (ARIPO), wamefanya Mkutano wa tano (5) wa Kikanda wa Afrika kuhusu masuala ya Hakimiliki na Hakishiriki katika kazi za vielelezo vya kusikia na kuona (5th African Regional Seminar on Copyright and Related Rights in the Audiovisual Sector) uliofanyika hoteli ya ONOMO Dar es salaam, Tanzania tarehe 15 Julai, 2026.
Mkutano huo umefunguliwa na Mwenyekiti wa Bodi ya COSOTA Ndugu. Victor Tesha ambapo umehudhuriwa na wageni kutoka nchini na wanachama wa Shirika la Kikanda la Miliki Ubunifu la Afrika (ARIPO) na baadhi ya nchi za Ulaya.
Lengo la Mkutano huu ni kuwajengea uwezo wadau wa Hakimiliki na Hakishiriki katika kushughulikia masuala yanayohusu kazi za vielelezo vya kusikia na kuona (audiovisual works), pamoja na kupata uzoefu kutoka nchi nyinngine kwenye masuala ya usimamizi wa kampuni za kukusanya na kugawa mirabaha katika kazi za filamu. Aidha Mkutano huu umepangwa kufanyika kwa siku mbili, tarehe 15 na 16 Julai, 2026
