Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
Utangulizi

 

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA)  ipo chini ya Wizara ya Utamaduni  , Sanaa na Michezo na imeanzishwa chini ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki na 7 ya Mwaka 1999. COSOTA ilianza rasmi mwaka 2001 ikiwa na majukumu makuu mawili , usimamizi wa Hakimiliki nchini  lakini pia  ukusanyaji na ugawaji mirabaha. Kufuatia mabadiliko ya Sheria ya fedha ya mwaka 2022 (Finance Act 2022) ilitenganisha majukumu hayo na kuanzisha makampuni binafsi  ya kukusanya na kugawa mirabaha nchini (CMO),ambapo kwa sasa Ofisi ya Hakimiliki imebaki kusimamia masuala ya Hakimiliki na kutoa leseni kwa Makampuni yanayohusika na kukusanya na kugawa mirabaha (CMO) pamoja na kusimamia masuala ya uharamia wa kazi za wabunifu