Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndg. Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Septemba 27, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 01 Septemba, 2023.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Hakimiliki Tanzania Bw. Victor Tesha (aliyesimama watatu kushoto) na pamoja na wajumbe wenzake mara baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo, uliyofanyika Septemba 12, 2023 Jijini Dar es Salaamu .
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimkabidhi Cheti cha Utambulisho wa Ubalozi wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania Msanii Barnaba Classic katika hafla ya Uzinduzi wa Bodi ya COSOTA na Bodi ya Bodi Filamu Septemba 12, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Taasisi zinazosimamia Miliki bunifu nchini COSOTA, BRELA, BPRA na COSOZA wakisaini makubaliano ya pamoja ya kuanzisha kituo cha kutoa elimu ya miliki bunifu nchini kwa kushirikiana na Shirika la Miliki bunifu Duniani (WIPO) katika hafla ya mgao wa mirabaha, pamoja na utoaji leseni kwa kampuni ya kukusanya na kugawa mirabaha kwa kazi za Muziki kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Hakimiliki ya mwaka 2022 yaliyoliondolea COSOTA jukumu la kukusanya na kugawa mirabaha na kuwaruhusu wabunifu wenyewe kufanya hilo, Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Haraza Chana akikabidhi hundi ya mfano ya mgao wa mirabaha kwa bendi ya Msondo ngoma katika hafla ya mgao wa mirabaha Julai 21 , 2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Said Yakub akikabidhi tuzo ya Shukrani kwa aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki wa pili wa COSOTA Bw. Yustus Mkinga katika hafla ya mgao wa mirabaha, utoaji leseni kwa kampuni ya kukusanya mirabaha kwa kazi za Muziki TAMRISO na utiaji saini makubaliano ya kuaznisha kituo cha kutoa elimu ya miliki bunifu baina ya COSOTA ,BRELA, COSOZA na BPRA Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare (wa kwanza kulia) akikabidhi Leseni kwa viongozi wa wa Kampuni ya kukusanya na kugawa Mirabaha kwa kazi za Muziki itwayo TAMRISO kufuatia mabadiliko ya sheria ya hakimiliki na hakishiriki iliyotaka wabunifu kukusanya mirabaha yao wenyewe na kujigawia na kulitoa jukumu hilo kwa COSOTA, katika hafla ya mgao wa mirabaha, Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Miliki Bunifu la Kikanda la Afrika (ARIPO) Amadu Bah (kulia) akikanidhi hundi ya mfano ya mgao wa mirabaha wa msanii Raymond Mwakyusa (Rayvanny) iliyopokelewa kwa niaba yake na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na mdau wa muziki Mhe. Shaban Hamis Taletale, katika hafla ya mgao wa mirabaha, Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Bima TIRA Dkt. Baghayo Saqwera (kushoto) akikabidhi hundi ya mfano ya mgao wa mirabaha wa msanii Nasibu Abdul (Diamondplatinumz) iliyopokelewa kwa niaba yake na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na Mdau wa muziki Mhe. Shaban Hamis Taletale, katika hafla ya mgao wa mirabaha, Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.