Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
Msaada wa Kisheria na Utatuzi wa Migogoro
Msaada wa Kisheria na Utatuzi wa Migogoro

Msaada wa Kisheria na Utatuzi wa Migogoro

Pamoja na majukumu mengine Ofisi ya Hakimiliki kupitia  Kitengo cha Sheria  inahusika na usuluhishi wa Migogoro mbalimbali inayohusu uvunjifu wa hakimiliki inayoletwa na wanachama katika  Ofisi ya  Hakimiliki (COSOTA).  

Utaratibu wa Kushuhulikia Lalamiko.

1.Mlalamikaji anatakiwa kumwandikia barua Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA kuhusu lalamiko  lake dhidi ya mtu binafsi au Taasisi ambayo anaona kwa namna moja ama nyingine imevunja haki zake za kiubunifu.

2. Mara baada ya kupokea barua ya lalamiko  idara huandaa barua ya wito kwa mlalamikiwa ili aweze kufika katika ofisi za Hakimiliki kujibu malalamiko dhidi yake ama kumpa muda wa siku zisizopungua saba ili aweze kujibia uhalali wa yeye kumiliki na kutumia kazi husuka.

3.Katika utatuzi wa migogoro ya kazi za wabunifu pande zote hukaa meza moja na maafisa wa sheria na wataalamu mbali mbali wa Hakimiliki ili kusuluhuhisha mgogoro huo,

4.COSOTA uhakikisha pande zote mbili zinamaliza tofauti zao kwa njia ya amani, na  iwapo mmoja wao hajaridhika na usuluhishi huo anaweza kwenda mahakamani  na COSOTA inaweza kwenda kutoa ushahidi wa kitaalamu.