MAJUKUMU YA OFISI YA HAKIMILIKI TANZANIA (COSOTA)
MAJUKUMU YA OFISI YA HAKIMILIKI TANZANIA (COSOTA)
MAJUKUMU YA OFISI YA HAKIMILIKI TANZANIA
Kwa mujibu wa kifungu cha 51 cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki, COSOTA majukumu ni :
- Kusaidia uanzishwaji wa kampuni za ukusanyaji na ugawaji mirabaha;
- Kutoa leseni na kusimamia uendeshwaji wa kampuni za ukusanyaji na ugawaji mirabaha (CMO)
- Kutunza rejista ya kazi za ubunifu (Sanaa na Maandishi);
- Kupambana na uharamia;
- Kutoa elimu ya hakimiliki;
- Kumshauri Waziri katika masuala ya hakimiliki;
- Kukusanya na kugawa mirabaha kwenye madaraja ambayo hayana CMO; na
- Kumshauri Waziri mwenye dhamana kuhusu masuala ya hakimiliki na hakishiriki.
KAZI ZINAZOLINDWA NA SHERIA YA HAKIMILIKI NA HAKISHIRIKI
-
- Vitabu, vitini na maandishi mengine ikiwa ni pamoja na programu za kompyuta;
- Mihadhara, hotuba, mahubiri na kazi nyingine zenye uelekeo huo;
- Kazi za drama na zile za muziki wa drama;
- Kazi za kimuziki (kwa sauti na ala) zenye kujumuisha au bila kujumuisha Maneno;
- Kazi za kikolegrafia na michezo bubu ya kuigiza;
- Kazi za upigaji picha za sinema na kazi zingine za vielelezo vya kuona na kusikia;
- Kazi za kuchora kwa kutumia rangi, usanifu wa majengo, sanaa ya uchongaji vinyago, sanaa ya uchongaji nakshi, sanaa ya litographia na mapambo;
- Kazi za sanaa ya kupiga picha ikiwa ni pamoja na kazi zinazotolewa kwa njia zinazoambatana na upigaji picha;
- Kazi za sanaa tumizi, ziwe kazi za mikono au zinazotengenezwa katika viwango vya viwandani; na
- Vielelezo, ramani, plan, michoro na kazi za mawanda matatu zinazohusiana na jiographia, topographia, usanifu wa majengo au sayansi.
