Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI, BAA NA MABASI WAPEWA SOMO LA KULIPA MIRABAHA
12 May, 2026
WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI, BAA NA MABASI WAPEWA SOMO LA KULIPA MIRABAHA

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Ishengoma awasihi watumiaji wa kazi za muziki kuipa ushirikiano kampuni ya kukusanya na kugawa mirabaha ya Society of Music Advocacy (SOMA) kwa kulipa mirabaha ili kuwasaidia Wasanii wa Muziki waweze kunufaika na kazi zao.

Kikao hicho kimefanyika leo Aprili 23,2026 na kililenga kutoa elimu ya umuhimu wa kulipa mirabaha kwa wadau mbalimbali ikiwemo wamiliki wa vyombo vya habari, wamiliki wa baa, kumbi za sherehe, kumbi za starehe, mabasi, madaladala na hoteli na migahawa.

Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA Bi. Naomi Mungure alifafanua kuwa jukumu la kukusanya na kugawa mirabaha hivi sasa linafanywa na kampuni binafsi za zilizoanzishwa na Wasanii wenyewe baada ya marekebisho ya sheria ya ya Hakimiliki na Hakishiriki yaliyofanyika Mwaka 2022 ambapo hivi sasa kuna kampuni mbili ambazo ni Tanzania Reproduction Rights Society inayokusanya kwa kazi za Maandishi na SOMA wanaokusanya mirabaha ya kazi Muziki.

Kikao hicho kimeandaliwa na COSOTA kwa kushirikiana na SOMA  kwa udhamini wa Alliance Francisie

slot gacor