VYONNE CHAKACHAKA ATEMBELEA OFISI ZA COSOTA
Mwana mziki mkongwe kutokea nchini Afrika Kusini Yvonne Chakachaka (katikati) ametembelea Ofisi za Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya COSOTA Bw. Victor Tesha (wapili kushoto) pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Bi Naomi Mungure(wapili kulia) kufahamu namna COSOTA inasimamia hakimiliki za wabunifu nchini.
Kikao hicho kililenga kujadili umuhimu wa ulinzi wa hakimiliki kwa kazi za wasanii na namna Afrika inahitaji kupambna kulinda kazi za wabunifu wake ili wanufaike zaidi, kwa kutoa elimu ya hakimiliki na umuhimu wa mikataba isiyokandamizi.
Msanii huyo mkongwe ameeleza uzoefu wake katika kusimamia hakimiliki za kazi zake kwa kusema kila kazi anayofanya anahakikisha anasaini makubaliano ya namna ya kunufaika na mirabaha.
Chakachaka atakuwa mgeni wa heshima kwenye kilele cha Jukwa la Mashariki Creative Economy Expro 2026 inayofanyika Mlimani City Jijini Dar es salaam kuanzia 18-21 Agosti, 2026.
Jukwaa hilo limebeba mkakati wa kuunganisha wabunifu na wasanii wa Afrika Mashariki pamoja katika kulinda kazi zao na kukuza masoko kujengeana uwezo wa fursa mbalimbali
