Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
COSOTA YAPONGEZWA KWA KUTATUA MGOGORO WA MFUMO WA TIRA MIS
24 Apr, 2023
COSOTA YAPONGEZWA KWA KUTATUA MGOGORO WA MFUMO WA TIRA MIS

Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare Aprili 20, 2023 ameshiriki kikao cha kubadilisha uzoefu cha  Umoja wa Wanawake Viongozi wa Taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali Tanzania, (Tanzania Women CEO's Roundtable chini ya Bi. Emma Kawawa) kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kililenga kubadilisha uzoefu kutokana na taasisi wanazozifanyia kazi na kuangalia namna bora ya taasisi hizo zinaweza kuwa na ushirikiano katika kuimarisha utendaji na Usimamizi wa majukumu ya Ofisi wanazozisimamia pamoja na wadau wake.

Akizungumza katika kikao hicho Doreen alielezea umuhimu wa usajili wa ubunifu kupitia miliki bunifu kwa ofisi za COSOTA na hata zinazosimamiwa na mwamvuli wa miliki ubunifu (Intellectual  Property) chino ya BRELA.  Alikumbusha masuala ya Hakimiliki katika mifumo na kazi mbalimbali zinazoandaliwa na taasisi na Ofisi zinazosimamia shughuli mbalimbali. Kwa sababu bunifu hizo zisiposajiliwa zinaweza kuleta mgongano  wa kimaslahi  na kuibua migogoro na hatimaye kupotea kwa haki.

Naye Mgeni Rasmi, Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware alitoa pongezi kwa COSOTA kwa namna walivyoweza kusimamia mgogoro wa taasisi yake uliyohusu mfumo wao wa TIRA MIS ambao kwa sasa umekua maarufu na muhimu sana katika masuala ya bima. Wawasilishaji na wadau walijadili pia kuhusu Uongozi, UTT, Institute of Directors Tanzania (IoDT), Vikoba na biashara mbali mbali