Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
COSOTA YATOA ELIMU YA HAKIMILIKI KWA WABUNGE YA WA KAMATI MBILI ZA BUNGE
22 May, 2023
COSOTA YATOA ELIMU YA HAKIMILIKI KWA WABUNGE YA WA KAMATI MBILI ZA BUNGE

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amefungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kwa Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo pamoja na Sheria Ndogo kuhusu Hakimiliki na Mabadiliko ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki .

Akizungumza katika ufunguzi huo Mhe. Balozi Dkt.Pindi amesema  lengo la Mafunzo hayo ni kupata uelewa wa usimamizi wa Hakimiliki na fursa za kibiashara katika masuala ya Hakimiliki, mafunzo hayo yamefanyika Leo Mei 18, 2023.

"Kamati hizi zimekua chachu katika kuboresha utekekezaji wa majukumu ya Wizara, hivyo tumeona ni vyema mafunzo haya yafanyike ili tuweze kushiriki mageuzi haya katika kukuza Sekta ya ubunifu nchini" amesema Mhe. Chana.

Aidha, Mhe. Pindi Chana ameushukuru Uongozi wa Bunge kwa kutoa nafasi kwa COSOTA kutoa mafunzo kwa Wabunge hatua inayowapa fursa ya kupata uelewa wa majukumu ya Taasisi na kuwaalika Wabunge hao kujenga tasnia ya Sanaa na Taifa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizarani hiyo, Bw. Said Yakubu amesema mafunzo hayo yatakua endelevu kwa Taasisi zote za wizara ili Waheshimiwa Wabunge waelewe vyema na kusaidia katika kukuza Sekta za Wizara.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi. Doreen Anthony Sinare amesema tayari Ofisi hiyo imeshatoa tangazo la Kampuni Ukusanyaji na Ugawaji Mirabaha kuomba Leseni za Kuanziasha kampuni hizo na mpaka sasa Kampuni moja ndiyo iliyoomba hivyo Ofisi inampango wa kuomba kibali kutoka Bodi ya Wakurugenzi ya kuomba kutangaza tena ili kutoa nafasi nyingine kwa wadau kuomba tena sababu wameomba kuongezewa muda ni kidogo ili kukamilisha mchakato.


Afisa Mtendaji Mkuu ameongeza kuwa Ofisi hiyo inajukumu la kutekeleza Ilani ya Chama Tawala ya 2020-2025 ambayo inasisitiza kusimamia wabunifu kunufaika zaidi na kazi zao zinazolindwa na Sheria ya Hakimiliki.


Pamoja na hayo nae Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Prof.Kitila Mkumbo alipongeza COSOTA kwa kuandaa mafunzo hayo kwa kushirikiana na wadau akiwemo Azam, DSTV na Ziiki, angependa mafunzo hayo ya Hakimiliki yatolewe kwa wabunge sababu ni muhimu sana.