Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
Mkutano wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika wa kujadili hakishiriki za Wasanii na Watayarishaji Nairobi
17 Apr, 2023
Mkutano wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika wa kujadili hakishiriki za Wasanii na Watayarishaji Nairobi

 

Afisa Hakimiliki Mwandamizi Naomi Mungure ashiriki Mkutano wa Nchi za Kusini mwa Sahara Afrika uliokuwa ukijadili usimamizi wa  Hakishiriki za wabunifu mbalimbali kama Wasanii, Watayarishaji na wadau wengine namna bora ya wao kunufaika na kazi zao.

Mkutano huo umefanyika Leo Machi 30, 2023 Jijini Nairobi nchini Kenya  na uliandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Kusimamia Hakishiriki za Watayarishaji, “International Federation of Phonographic Industry - IFPI".

Katika mkutano huo Afisa Hakimiliki huyo aliwasilisha taarifa ya Mabadiliko ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 2022 na kueleza hivi karibu Tanzania inakwenda kuanzisha Makampuni ya Ukusanyaji na Ugawaji wa Mirabaha (CMO's), lakini pia alieleza ushirikiano mzuri ambao COSOTA inapata kutoka serikalini.

Mkutano huo umezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo umuhimu wa mahusiano mazuri na serikali kwa makampuni ya kukusanya na kugawa Mirabaha,katika uwazi wa masuala ya fedha na viwango vya malipo ya Leseni za matumizi ya kazi za ubunifu na  mkakati wa  kuwa na CMO'S bora  katika nchi za Afrika.

Pamoja na hayo walijadili umuhimu wa CMO kushirikiana vizuri na Ofisi za Hakimiliki na kuwa na mahusiano mazuri na wadau na wenye hakimiliki ili Wasanii waweze  kunufaika na kazi zao.