Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
MSIGWA AITAKA COSOTA KUONGEZA MAPATO NA KUANDAA MIRADI
01 Nov, 2023
MSIGWA AITAKA COSOTA KUONGEZA MAPATO NA KUANDAA MIRADI

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg.Gerson Msigwa atoa maelekezo kwa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuongeza vyanzo mapato pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali itakayosaidia kuboresha utekelezaji wa majukumu.

Mheshimiwa Msigwa ametoa maelekezo hayo  Oktoba 31, 2023 katika kikao chake na Menejimenti ya COSOTA alipotembelea Ofisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.

"Katika kipindi cha uongozi wangu ninahitaji sana kuona Wizara na Taasisi zinaonekana na zinasema utekelezaji wa shughuli zake, na kwa upande wa COSOTA mnahitaji kujitangaza zaidi na kutoa elimu masuala haya ya hakimiliki bado jamii haijui vizuri mnakazi kubwa katika kutekeleza hili" alisema Msigwa.

Akiendelea kuzungumza Katibu Mkuu huyo alishauri COSOTA kutazama Sheria kama inaruhusu  ili kuweza kufikiria suala la kupambana na uharamia utekelezaji wake ufanywe Kampuni binafsi kwa usimamizi wa COSOTA  ili kuweza kutekeleza kwa ufanisi jukumu hilo kwa Tanzania nzima na kudhibiti watu  wanaofanya shughuli hizo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Bi. Doreen Anthony Sinare alimshukuru Katibu Mkuu huyo na kupokea maelekezo na ushauri ambapo aliahidi kuyafanyia kazi na kutoa mrejesho.

Halikadhalika Doreen alieleza kuhusu Tozo ya Hakimiliki kuwa makusanyo yameanza tarehe 01.09.2023 kwa ushirikiano na TRA ambayo vifaa vilivyoingizwa bado ni vichache na aliomba nyongeza ya vifaa vingine ambavyo vinaendana na wakati wasasa kuongezwa ili kusaidia ongezeko la makusanyo na kuboresha mapato ya serikali, wasanii, waandishi na wabunifu mbalimbali katika masuala ya hakimiliki.izara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.