Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
Naibu Spika Bunge la JMT aipongeza Wizara ya Utamaduni
01 Jul, 2023
Naibu Spika Bunge la JMT aipongeza Wizara ya Utamaduni

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Musa Azzan Zungu (Mb) akiwa  ametembelea banda la Ofisi ya Hakimiliki Tanzania  Juni 30,2023 katika Maonesho ya Biashara ya 43 yanayofanyika uwanja wa  TANTRADE  Jijini Dar es Salaam .

Akizungumza katika ndani ya banda hilo Naibu Spika huyo aliipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na taasisi zake kwa kazi nzuri wanayofanya ya kusimamia na kuendeleza sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini na hivi sasa kuna mabadiliko mengi.

'Natoa pongezi za kipekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uhamasisha Michezo na kusimamia Utamaduni na Sanaa kwani amekuwa kiongozi wa mfano na ameacha alama katika kuhakikisha utamaduni wa Tanzania unalindwa na kuheshimiwa na kusimamia suala la wasanii kunufaika na kazi zao,' alisema Zungu.

Pamoja na hayo nae Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Said Yakub alimshukuru Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutembelea banda hilo.

kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa TANTRADE Bi.Latifa Khamis alipongeza wizra hiyo kwa maandalizi mazuri ya maonesho hayo pamoja na kuwa ni mara ya kwanza kwa wizara na baadhi ya taasisi zake kushiriki maonesho hayo ya Biashara ya Sabasaba.