Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
Ofisi ya Hakimiliki Tanzania ya Jibu hoja za Mwenyekiti wa TUMA
17 Apr, 2023
Ofisi ya Hakimiliki Tanzania ya Jibu hoja za Mwenyekiti wa TUMA

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania(COSOTA) leo Aprili 14,2023  imefanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Tanzania Urban Music Association (TUMA)  kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa hoja alizoibua Mwenyekiti wa TUMA Bw. Mike Tee katika post yake ya Instagram ya tarehe Aprili 10, 2023 iliyohoji kuhusu ripoti ya ukaguzi wa hesabu za COSOTA na CAG, Mgao wa Mirabaha na Makusanyo ya Mirabaha yanavyofanyika pamoja na namna Mgao wa Mirabaha unafanyika.

Akizungumza katika kikao hicho Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare alifafanua kuwa kuwa COSOTA kama Ofisi ya Serikali imekuwa ikikaguliwa na CAG na  taarifa ya ukaguzi wa hesabu za hizo niyawazi  CAG na taarifa hizo zinapatikana katika tovuti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

 "Kuhusu suala la COSOTA kuendelea kukusanya mirabaha kwa sasa, ni sehemu ya utekelezaji wa  Sheria kama ilivyoelekeza na jukumu la kukusanya litakabidhiwa kwa Kampuni za kukusanya na kugawa Mirabaha (CMO's) mara baada ya kufanya mgao wa mwezi Juni, 2023 na kuanzia mwezi Jula, 2023 CMO's ambazo zitakuwa zimekidhi vigezo zitaanza kazi ya kukusanya na kugawa Mirabaha hiyo,"alisema Doreen.

Pamoja na hayo Doreen alifafanua pia kuhusu makusanyo ya Mirabaha na Mgao kuwa COSOTA imekuwa ikitamani kufanya mgao mkubwa ili wabunifu waweze kunufaika na kazi zao. Lakini changamoto ni kwamba wengi wa watumiaji wa kazi hizo wamekuwa hawalipi na pamoja na kwamba operesheni zimekuwa zikifanyika, hivyo aliwasihi wadau hao kuungana  na COSOTA katika kipindi cha hivi karibuni kupaza sauti ili kuweza kuhamasisha watumiaji kulipa leseni ya matumizi ya kazi za Muziki katika maeneo ya biashara.

Naye Mwenyekiti wa TUMA Mike Tee  na timu nzima waliahidi kutoa ushirikiano katika kuhamasisha makusanyo ya mirabaha kwa kushirikiana na Wanachama wenzao  kupaza sauti kwa maeneo ambayo hayalipi yalipe ili mgao ujao uweze kuwanufaisha wadau wengi na wapate viwango  vikubwa zaidi.

Halikadhalika Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki huyo alitoa wito kwa wadau wa Sanaa na wabunifu kuwa huru  kutembelea COSOTA na kuuliza chochote kwa jambo lolote ambalo wangependa kupata ufafanuzi.