TAALUMA YA KUKUSANYA NA KUGAWA MIRABAHA
Kaimu Afisa Mtendaji COSOTA Bi. Naomi Mungure ameongoza kikao cha pamoja cha kupata uzoefu wa kitaalamu kuhusu taratibu za ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha kwa kampuni zinazokusanya katika kazi za Muziki na kazi za vielelezo vya kuona nakusikia (Audiovisual) kutoka Shirika la Kimataifa la Sekta ya Rekodi za Muziki (IFPI) Septemba 02, 2026
Kikao hicho kimefanyika jijini Dar es Salaam katika Makao Mkuu ya Ofisi za COSOTA ambapo Ofisi ya IFPI iliwakilishwa na Bw. Adipo Otieno.
Hivi karibuni COSOTA litoa leseni kwa kampuni ya Tanzania Audiovisual Collection (TAVIC) itakayokusanya ikikusanya mirabaha ya "Audiovisual" na kuhuiisha leseni ya kampuni ya Society of Music Advocacy (SOMA) inayokusanya mirabaha ya kazi za Muziki.
Kikao hicho kilihususisha kampuni hizo zote mbili kwa lengo la kupata uzoefu kutoka nchi mbalimbali na kushauri kwa kampuni hizo ya namna bora ambayo wanaweza kukusanya mirabaha katika maeneo ambayo wanaoingiliana bila kuleta changamoto kwa watumiaji wa kazi hizo.
