Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
TAMRISO KUKUSANYA MIRABAHA YA KAZI ZA MUZIKI KUANZIA JULAI 2023
30 Jul, 2023
TAMRISO KUKUSANYA MIRABAHA YA KAZI ZA MUZIKI KUANZIA JULAI 2023

Kuanzia mwakani Mirabaha itakusanywa na Wasanii wenyewe na Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) itabaki kama msimamizi.

Hayo yamesemwa leo Julai 21,2021 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakub katika tukio la ugawaji mirabaha linalofanyika hoteli ya  Jijini Dar es Salaam.

Amesema wasanii hao watakusanya mirabaha yao kupitia kampuni waliyoiunda inayoitwa Tanzania Music Right Society (TAMRISO).

Baadhi ya wasanii waliotajwa kuwepo katika kampuni hiyo yenye watu 30 ni pamoja na Nandy, P.Funk, Fid Q, Aslay, Babu Tale, Abby Chams, Sarafina na Profesa Jay.

Pia wapo Chama cha Muziki wa Dansi (Chamudata), chama cha muziki wa taarabu na waandaji mbalimbali wa muziki.