Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
WASANII SAJILINI MAJINA YENU YA KISANII KAMA ALAMA YA UTAMBULISHO WA BIASHARA ILI MNUFAIKE ZAIDI
05 May, 2023
WASANII SAJILINI MAJINA YENU YA KISANII KAMA ALAMA YA UTAMBULISHO WA BIASHARA ILI MNUFAIKE ZAIDI

Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare asisitiza Wasanii kuhakikisha wanasajili majina yao ya usanii kama "brand" ilikuweza kunufaika zaidi.

Doreen ametoa msisisitizo huo leo Aprili 28,2023 Jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa wadau wa wanaojihusisha na shughuli za ubunifu  katika Maadhimisho ya Siku ya Miliki Bunifu Duniani yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) katika mjadala wa Mada iliyokuwa inahusu mfumo WA usajili wa ulinzi wa Miliki Bunifu.

"Ofisi ya hakimiliki inafanya shughuli mbalimbali ikiwemo usajili wa kazi zote za ubunifu kama kazi za Maandishi, Filamu, Muziki, Mifumo  pia usuluhishi wa migogoro ya hakimili pamoja na kutoa huduma za ushauri wa kisheria katika mikataba na pale mbunifu kazi yake inapotumika bila ridhaa yake na akawasikisha mgogoro wake Ofisi ya COSOTA na ikafikia kuwa anakwenda mahamani huwa tunakuja kutoa ushahidi mahakamani ," alisema Doreen.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki ameeleza kuhusu la Mabadiliko ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 2022 ambapo wabunifu wanakwenda kukusanya na kugawa Mirabaha wenyewe na Kanuni ya

Pamoja na hayo COSOTA imepongezwa na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Saudin Mwakaje katika mkutano huo kwa kutajwa na Shirika la Kimataifa la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) katika jarida lao kuwa moja ya taasisi inayofanya vizuri katika Usuluhishi wa migogoro ya uvunjifu wa hakimiliki kwa kushughulikia mengi migogoro  na kuimaliza ndani ya ofisi bila ya wadau hao kwenda mahakamani.

Halikadhalika ilielezwa kuwa hakimiliki ni haki ni haki ya kipekee ambayo mbunifu anaipata mara baada ya kubuni kazi yake hata kabla ya kuisajili na Sheria inamlinda, ila ni muhimu sana kwa mbunifu kusajili kazi yake ili kuweza kutambulika kama mbunifu halali.

Kauli mbiu ya mwaka 2023  ya Maadhimisho ya Siku ya Miliki Bunifu Duniani ni "Wanawake na Miliki  Ubunifu Kuongeza Kasi ya Ubunifu katika Biashara".