Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
Wasanii wapatiwa Mafunzo ya namna ya Kusimamia Mtandao wa Youtube na kuweza kunufaika
24 Apr, 2023
Wasanii wapatiwa Mafunzo ya namna ya Kusimamia Mtandao wa Youtube na kuweza kunufaika

Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare leo Aprili 21, 2023 ameshiriki mafunzo kwa njia ya mtandao pamoja na baadhi ya Wasanii wa Tanzania na Maafisa wa COSOTA.

Mafunzo hayo yalikuwa yameandaliwa na vyama dada vya hakimiliki vya SAMRO na CAPASSO kutoka Afrika ya Kusini, mafunzo hayo yalilenga kutoa elimu ya namna Wasanii wanaweza kusimamia akaunti zao za  Youtube na kuweza kujipatia kipato bila ya  kulazimika kupitia kwa "aggrigetor" na mambo ya kuzingatia katika kupandisha katika mtandao.

Akizungumza katika kikao hicho Mtaalamu wa Youtube Bw. Eric Knapp alieleza ni muhimu Msanii anapokuwa na akaunti ya Youtube kuweka wasifu wake, na kuwa makini anapopandisha kazi yake kwa kuchagua anasambaza kazi yake katika jukwaa gani la Youtube, pia ni vyema kufanya uchambuzi wa mashabiki  wako wengi wanatokea wapi ili uweze kujua wapi unamashaniki wengi, pia kuhakikisha akaunti inakuwa na content mapya mara kwa mara.

"Unaweza kutengeneza wimbo wako ukauwekea "audio visual", au kuweka mashairi lengo ikiwa ni kuendelea kusambaza kazi yako zaidi, pia yapo matangazo ambayo yanapokuwa yametazamwa katika akaunti yako unapata kipato,  yapo mambo mengi ndani ya mtandao wa Yotube wasanii wakiyazingatia wanapata faida zaidi," alisema Knapp.

Pamoja na hayo Doreen aliendelea kutoa wito kwa wasanii kuacha kupuuza pale wanapopewa mwaliko wa kushiriki mafunzo kama hayo kwani wengi wanaweza kudhani wanafahamu sana Youtube lakini, kwa elimu iliyotolewa  ni kubwa na inaondoka changamoto ya wadau wengi wanazolalamika wakitumia 'aggrigetors'.

Aidha, nae Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Muziki Tanzania na Msanii wa Muziki wa Taarab Mzee Yusuph ameishukuru COSOTA kwa mafunzo hayo na kueleza kupitia mafunzo hayo ameweza kufanya maboresho ya akaunti yake wakati wa mafunzo na amejifunza vitu vingi ambavyo alikuwa havijui na ameomba COSOTA kuendelea kutoa elimu hiyo.

Halikadhalika mmoja wa Wadau wa Muziki Bw. Alponce Peter alielezea kuwa Wasanii wengi hawamjui namna wanaweza kunufaika na akaunti zao sababu wanaona ili waweze kunufaika nilazima akaunti isimamiwe na 'aggrigetor' na ni kwa sababu hawapendi kujifunza vitu mbalimbali.