Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
BILIONI 1.3 KUGAWIWA KWA WASANII NOVEMBA 26
18 Nov, 2026
BILIONI 1.3 KUGAWIWA KWA WASANII NOVEMBA 26

Mgawo wa Tozo ya Hakimiliki  kufanyika Novemba 26, 2026 ambapo kiasi cha bilioni 1.3 kugawiwa kwa Wasanii wa Muziki, Filamu, Sanaa za Maonesho, Sanaa za Ufundi na Kazi za Maandishi.

Taarifa hiyo imetolewa leo Novemba 17, 2026 jijini Dar es Salaam na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA Bi.Naomi Mungure alipokuwa akizungumza na  na Waandishi wa Habari kuhusu mgawo huo.

" Tozo ya Hakimiliki (Copyright Levy)  imeanzishwa kupitia mabadiliko ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki yaliyofanyika katika Sheria ya Fedha ya Mwaka 2022,"alisema Bi. Mungure.

Pamoja na hayo Bi. Mungure alifafanua kuwa Tozo hiyo imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa vifaa tupu vinavyoingia nchini au kuzalishwa vyenye uwezo wa  kuzalisha, kunaliki, kuhifadhi au kusambaza kazi za Wasanii na Wabunifu.

Vifaa vilivyotumika kukusanya tozo hiyo ni  CD, DVD, DIGITAL Juke bx, MP3 Player, SD Memory Card, Viny, MINI DISC,COMPACT DISC, RADIOSET ENABLING RECORDING, TV SET ENABLING, ANALOGUE AUDIO RECORDERS na ANALOGUE VIDEO RECODER .

Vilevile Tozo hiyo ipo katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Kenya, Malawi, Algeria, Ghana, Tunisia, Burkinafaso, Morocco, Marekani, Canada, Ufaransa, Australia, Ujerumani n.k.

slot gacor