KAMPUNI YA SOMA NA TAVIC ZA PATA SULUHU YA UTARATIBU WA KUKUSANYA MIRABAHA KATIKA MAENEO YENYE MWINGILIANO
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Ishengoma aongoza kikao cha kupata suluhusho ya mwingiliano wa maeneo katika ukukusanyaji wa mirabaha kwa Kampuni ya kukusanya na kugawa mirabaha ya Tanzania Audiovisual Collection (TAVIC) na Society of Music Advocacy (SOMA).
Kikao hicho kimefanyika Novemba 06, 2026 katika ofisi za COSOTA jijini Dar es salaam kwa lengo la kusaidia kampuni hizo kuweza kukusanya mirabaha katika maeneo yenye mwingiliano bila kuleta changamoto kwa watumiaji wa kazi hizo.
"Kampuni ya TAVIC kwa mujibu wa Sheria inakusanya mirabaha katika maeneo yenye matumizi ya kazi zenye vielelezo vya kusikia na kuona na kuna changamoto ya mwingiliano wa maeneo hivyo ni vyema tukakubaliana utaratibu mzuri wa kukusanya fedha hizo ili kuweza kufanikiwa kuwasaidia wasanii kunufaika na kazi zao," alisema Dkt. Ishengoma .
Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bi. Naomi Mungure alifafanua kuwa ni vielelezo vya kusikia na kuona ni kama Tamthiliya, Maigizo na Filamu.
Baada ya ufafanuzi huo Bi. Mungure aliwasilisha maeneo ya kukusanya mirabaha na kampuni hizo zilichambua na kugawa ili kuondoa mwingiliano katika ukusanyaji wa mirabaha.
Pamoja na hayo Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Sanaa na Ubunifu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Asha Salim alipongeza kampuni ya TAVIC kwa ubunifu wa kutuma jumbe fupi kwa wamiliki na biashara zinazotumia kazi hizo na alishauri kampuni hizo mbili kuwa zinaweza kuungana katika kutuma ujumbe mmoja .
Vilevile wito ulitolewa kwa COSOTA kutangaza kampuni hizo za kukusanya na kugawa mirabaha kwa umma.
