UMOJA MOVIE WASISITIZWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA HAKIMILIKI KATIKA UKAGUZI
Afisa Hakimiliki Mkuu, Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bw. Paul Makula atoa ufafanuzi wa majukumu ya Umoja Movie Distribution, kwa kueleza kuwa ni Kampuni inayofanya kazi ya usambazaji wa kazi za filamu na Kampuni hiyo imesajili kazi zake COSOTA hivyo kampuni hiyo inauwezo wa kumshtaki mahakamani mtu yoyote atakayekutwa anasambaza kazi hizo bila kuwa na ridhaa ya wamiliki hao.
Bw. Makula ameyasema hayo Novemba 04, 2026 jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa Waandishi uliondaliwa na Umoja Movie wa kuwatambulisha mabalozi wake na kuelezea shughuli wanazozifanya.
Vilevile Afisa huyo wa COSOTA amewasisitiza viongozi wa kampuni hiyo kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Hakimiliki wakati wakifanya ukaguzi wa kazi zao.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Umoja Movie Distribution Bw. Idrisan Yasin Lihuwi amesema lengo kuu la kampuni hiyo ni kukuza soko la tasnia ya filamu hasa kupitia Maktaba za video (Video Library) na wanampango wa kuandaa mikataba ya biashara ya filamu kati ya kampuni yetu na wasambazaji wadogo.
"Katika kila Mkoa tunamawakala wetu ambao na simamia usambazaji wa kazi zetu na kufanya ufuatiliaji wa kwa wale wanaosambaza kazi zetu bila kuzingatia utaratibu, na mawakala hao wanatambulika kwa vitambulisho rasmi vya Umoja Movie" alisema Bw. Lihuwi.
Bw. Lihuwi amewambulisha rasmi kwa umma mabalozi wa Umoja Movie Distribution ambao ni Daudi Tairo maarufu kama Duma, Madebe Athumani maarufu kama Madebe, Musa Mahenge maarufu kama Kitale na Derick Gerald maarufu kama Nyuki.
Pamoja na hayo naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Audiovisual Collection (TAVIC) Bw. Fadhili Mfate nae alifafanua kuwa Mabalozi wa Umoja Movies ni sehemu ya wadau wa TAVIC, hivyo wanasaidia katika kushauri maswala mbalimbali ya kukusanya na kugawa mirabaha ndani ya kampuni.
