Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
COSOTA YAFANYA KIKAO NA SOMA
03 Oct, 2026
COSOTA YAFANYA KIKAO NA SOMA

Maafisa wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) wamefanya kikao cha ufuatiliaji wa utekelezaji wa majukumu na  Kampuni ya kukusanya na kugawa mirabaha Society of Music Advocacy (SOMA) katika daraja la vielelezo vya kusikia.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 02 Oktoba, 2026 jijini Dar es salaam na kufanya mazunguzo na Mkurugenzi wa kampuni ya kukusanya na kugawa mirabaha SOMA Bw. Hermes Joachim kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali ikiwemo makusanyo na mgao wa mirabaha, usajili wa wanachama na utoaji leseni kwa wanachama.

 Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa SOMA Bw. Hermes Joachim alisema wametengeneza mfumo wa kidigitali utakaokuwa unanasa nyimbo za wasanii zitakazokuwa zinarushwa na redio mbalimbali nchini ili uweze kuwasaidia katika ugawaji wa mirabaha, mfumo huo upo katika hatua ya majaribio na unategemea kunza kufanya kazi rasmi mwaka 2027.

Aidha, kampuni hiyo imeweza kufikia wasanii wakongwe na wasanii wapya  nchini kupitia mabalozi wao ambao ni Fareed Kubanda (Fidq),  Abdullaziz  Chande (Dogo janja), Kheri Rajabu (Mr. Blue), Charles (Chamu Charles) Baba n.k 

"Kupitia Tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva kwa mwezi Septemba, 2026 tumesajili Wanachama 120 na  kazi 390,"alisema Bw. Hermes.

Pamoja na hayo COSOTA imekubaliana na SOMA kuanzisha Podcast ya kutoa elimu ya hakimiliki na kurekodi kipindi kitakachorushwa katika vyombo vya habari.

Halikadhalika kampuni ya SOMA inafanya kazi ya kukusanya mirabaha katika vyombo vya habari, vyombo vya usafiri, hotelini, kumbi za starehe, taasisi za fedha (bank) n.k.

Maafisa walioshiriki katika kikao hicho ni Bw. Posper Massawe kutoka  Kitengo cha Uzingatiaji, Bi. Rhoda Lupondo kutoka Kitengo cha Leseni na Uharamia pamoja na Bi Anitha Jonas kutoka Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano.

slot gacor