WATUMISHI WA COSOTA WASHIRIKI MAFUNZO YA MFUMO WA WIPO
Maafisa wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Bi. Mwanaasha Sendekwa na Bw. Samwel Alfred, wameshiriki mafunzo ya mfumo wa WIPO Connect unaomilikiwa na Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) yaliyofanyika katika Ofisi ya Hakimiliki Zanzibar (COSOZA), tarehe 28 Septemba - 1 Oktoba 2026.
Lengo la ushiriki wa mafunzo hayo ni kujifunza namna mfumo huo unafanya kazi ili kuweza kuboresha mfumo wa COSOTA wa usajili wa kazi (CRMIS).
Mafunzo hayo yalitolewa na Mshauri Mwandamizi wa Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) Bw. Boukary Sawadogo kutoka nchini Burkina Fasso.
Mfumo huo wa WIPO connect unafanya kazi mbalimbali ikiwemo usajili wa kazi, kugawa mirabaha, utafutaji na uhakiki wa taarifa za kazi, utambuzi wa wamiliki wa haki, pamoja na ulinganishaji wa taarifa za kazi.
Ushiriki huo ni sehemu ya jitihada za COSOTA za kuimarisha uwezo wa watumishi wake na kuboresha matumizi ya mifumo ya kisasa katika usimamizi wa hakimiliki na hakishiriki nchini.
