Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
COSOTA YAITEMBELEA TANRRS
25 Sep, 2026
COSOTA YAITEMBELEA TANRRS

Maafisa wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) watembelea ofisi ya Kampuni ya Kampuni ya Kukusanya na Kugawa Mirabaha ya Tanzania Reproduction Rights Society (TANRRS) inayokusanya mirabaha kwa kazi za daraja la maandishi.  
​Maaafisa hao wametembelea kampuni hiyo Septamba 24, 2026 na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Abdallah Saiwad kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali ikiwemo hatua za makusanyo ya mirabaha, usajili wa wanachama na mpango wa kampuni hiyo katika kujitangaza ili kuweza kufikia wadau wengi pamoja na kufahamu changamoto wanazopitia ili COSOTA waweze kuwasaidia.  
​Pamoja na hayo kampuni hiyo ilisisitiza kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari ili kuweza kufahamika nchini na kuwafikia wadau wengi watakaonufaika na matumizi ya kazi zao.  
​Kampuni hiyo inakusanya mirabaha kwa katika Vyuo Vikuu, Vyuo vya Kati na Stationaries ( Ofisi zinazotoa nakala (copy) za vitabu,  
​Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya usimamizi wa COSOTA kwa kampuni za kukusanya na kugawa mirabaha.

slot gacor