Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
MHE. WAZIRI MAKONDA-BILIONI MBILI MGAO WA MIRABAHA MWEZI NOVEMBA 2026
25 Sep, 2026
MHE. WAZIRI MAKONDA-BILIONI MBILI MGAO WA MIRABAHA MWEZI NOVEMBA 2026

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda (Mb), ametangaza mgawo wa mirabaha ya Tozo ya Hakimiliki inayosimamiwa na Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kufanyika Novemba 2026 ambapo kiasi cha shilingi bilioni mbili  kitagawiwa.

Mheshimiwa Waziri Makonda ameyasema hayo Septemba 24, 2026 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) na Shindano la Urembo la Dunia (Miss World 2027).

​ "Wasanii walioshiriki Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva wanahitaji kuona faida ya matumizi ya kazi zao na kupata matunda halisi ya jasho lao," alisema Mhe.Makonda.

​Pamoja na hayo Mhe. Makonda alieleza utayari wa nchi katika kuandaa AFCON 2027 na alieleza kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa viwanja pamoja na kutoa elimu kwa watanzania ya kuchangamkia fursa mbalimbali katika msimu huo ili kuifanya Tanzania kuwa nchi mwenyeji ya mfano katika mashindano hayo kwa kufungua fursa za kiuchumi na kutangaza sekta ya utalii.

​Aidha, kuhusu hoja ya jezi ya timu ya taifa ya mpira wa miguu  iliyozinduliwa hivi karibuni, Waziri Makonda aliendelea kusisitiza kuwa jezi hiyo haina kiwango pia mchakato wa utayarishaji wa jezi hiyo haukuzingatia masharti ya mkataba aliyopewa mtoa huduma.

Halikadhalika Mhe. Makonda alitoa wito kwa Watanzania na Wanahabari kuendeleza mijadala yenye tija itakayosaidia kukuza vipaji na kuleta maendeleo endelevu katika Sekta ya Sanaa na Michezo.

slot gacor