RAIS SAMIA APEWA TUZO YA HESHIMA
RAIS SAMIA APEWA TUZO YA HESHIMA
27 Nov, 2026
Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imetoa tuzo ya heshima kwa Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sana na Utamaduni Ndg. Methusel Ntonda kwa uongozi imara katika kuendeleza sekta ya ubunifu na sanaa kwa kuanzisha tozo ya hakiiliki inayonufaisha wabunifu nchini.
Tozo ya Hakimiliki (Copyright Levy) ni tozo maalum inayotozwa kwenye vifaa vya kielektroniki vinavyoingizwa nchini ambavyo vinauwezo wa kurikodi, kuzalisha, kunakili, kuhifadhi au kusambaza kazi za sanaa na ubunifu kama vile CD, DVD, Memory Card, Vinyl n.k kwa lengo la kuongeza chanzo cha mapato kwa wabunifu na wasanii.
