Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
COSOTA YAKUSANYA BILIONI MBILI YA TOZO YA HAKIMILIKI
27 Nov, 2026
COSOTA YAKUSANYA BILIONI MBILI YA TOZO YA HAKIMILIKI

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Bi. Naomi Mungure, akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mirabaha ya tozo ya  hakimiliki iliyokusanywa na   kumkaribisha Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Methusela Ntonda. 

Katika hotuba ya Bi. Mungure ya Novemba 26, 2026 alieleza madhumuni ya kuanzishwa kwa Ofisi ya hakimiiki na  majukumu ya Ofisi hiyo katika kusimamia, kulinda na kuhakikisha haki za kiuchumi za wabunifu zinatambuliwa, pamoja na hatua iliyofikiwa katika ukusanyaji wa mirabaha inayotokana na matumizi ya kazi za wabunifu katika maeneo mbalimbali. 

Aidha, alieleza kuwa COSOTA imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Bilioni 2 za mirabaha na kwamba hafla hii ni ya kihistoria kwa Ofisi ya hakimiliki ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa ukusanyaji wa mirabaha ya tozo ya hakimiliki kufanya ugawaji kwa wabunifu, hatua inayodhihirisha mafanikio katika utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa hakimiliki nchini. 

Ugawaji huu ni hatua muhimu katika kuhakikisha wabunifu wanapata stahiki zao, kutambua thamani ya kazi zao na kuimarisha mfumo wa hakimiliki unaochochea ukuaji wa sekta ya ubunifu nchini.
 

slot gacor