Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
COSOTA YASHIRIKI MKUTANO ULIOANDALIWA NA CISAC NA ADGP
11 Sep, 2026
COSOTA YASHIRIKI MKUTANO ULIOANDALIWA NA CISAC NA ADGP

COSOTA, kupitia Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Bi. Naomi Mungure, ilishiriki mkutano ulioandaliwa na CISAC pamoja na ADAGP (Copyright Society in the Visual Arts - Paris), na baadhi ya CMOs kuhusu usimamizi wa haki za sanaa za ufundi (Visual Arts), ikiwemo haki ya msanii kunufaika na mauzo ya pili au zaidi ya kazi zake za sanaa (Resale Right). Uuzwaji huu ni kama uuzaji wa picha zilizochorwa (paintings) kwenye minada iitwayo "Resale right" ambayo Tanzania imeweka utaratibu kuwa kila kazi inapouzwa katika minada, asilimia fulani inatakiwa kulipwa kwa Msanii husika.
​Hii inatekelezeka pale ambapo nchi zote mbili zina vifungu hivi katika Sheria na inatekekezwa katika nchi husika.
​Baada ya mkutano, Bi. Naomi alikutana na Marie-Anne Ferry-Fall, Afisa Mtendaji Mkuu wa ADAGP, ambapo pande hizo zilikubaliana kuanza ushirikiano rasmi kupitia makubaliano yatakayowezesha usajili wa kazi, ukusanyaji na ugawaji wa mapato ya wasanii wa sanaa za ufundi.
​Mkutano pia ulijadili ugawaji wa mirabaha na mapato ya Tozo ya Hakimiliki (Copyright Levy), ambapo Tanzania imekusanya Shilingi 2.22 bilioni kati ya Septemba 2023 na Aprili 2026.
​COSOTA inatarajia kuanza utekelezaji wa mfumo huu kwa kushirikiana na wasanii, wataalamu wa biashara ya sanaa (arts professional dealers), CISAC, balozi mbalimbali, (kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Mambo ya Nje).
​Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Bi. Doreen Sinare, Samuel Sangwa Mkurugenzi wa CISAC Afrika na wawakilishi wa World Intellectual Property Organization (WIPO)

slot gacor