MAADHIMISHO SIKU YA MUZIKI DUNIANI
Afisa Hakimiliki Bi. Martha Urio ametoa elimu kwa wasanii wa muziki katika maadhmisho ya siku ya muziki duniani katika viwanja vya Azimio la Arusha (Arusha declaration) jijini Arusha, kwa kusisitiza wasanii kutambua haki zao hasa wakati wa kuingia makubaliano mbalimbali.
Maadhmisho haya yameratibiwa na Tanzania Music Foundation (TAMUFO) kuanzia tarehe 09 hadi 11 Oktoba, 2026 katika viwanja vya Azimio la Arusha, ikiwa na kauli mbiu “Muziki wetu Taifa letu na Amani yetu”
Halikadhalika Taasisi ya Youth Grow Foundation imesaidia vijana wengi kujitambua na kupata fursa ya kuchimba madini maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Aidha Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikua diwani wa kata ya Ngarenaro Bw. Abdulazizi Abubakar Chande (Dogo janja) akimuwakilisha Meya wa jiji la Arusha ambae pia ni diwani wa kata ya Kaloleni Bw. Maximilian Matle Irange.
Pamoja na hayo TYF wameomba maafisa utamaduni wa jiji na mkoa wa Arusha waweze kuwasaidia wakutane na wasanii wa mkoa huu ili kukuza vipaji vya wasani hao.
