MGAO WA KWANZA WA TOZO YA HAKIMILIKI
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Methusela Ntonda akimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Christian Makonda, ameipongeza Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) pamoja na kampuni za kukusanya na kugawa mirabaha (CMOs) kwa juhudi za kukusanya na kugawa mirabaha kwa wabunifu.
Mgao huo umefanyika Novemba 26, 2026 katika ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
Bw. Ntonda amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kukuza na kuendeleza tasnia ya sanaa nchini kupitia ujenzi wa mazingira wezeshi kwa wabunifu.
Aidha ameeleza kuwa hatua hizo ni pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, unaotoa mikopo kwa wasanii kwa riba nafuu ili kuwawezesha kukuza shughuli zao za kisanaa na kiuchumi.
Bw. Ntonda amewapongeza wabunifu waliojisajili COSOTA na kusisitiza umuhimu wa usajili huo katika kulinda haki zao na kuhakikisha wanapata stahiki zinazotokana na matumizi ya kazi zao za ubunifu.
