SHULE YA SEKONDARI MAKONGO YASHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA YA MILIKI UBUNIFU ZIMBABWE
Shule ya Sekondari Makongo yashiriki mashindano ya Kimataifa ya Miliki Bunifu yaliyofanyika nchini Zimbabwe tarehe 29 Mei, 2026 mashindano hayo yaliratibiwa na Ofisi ya Hakimiliki Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Miliki Bunifu la Kikanda la Afrika (ARIPO) .
Mashindano hayo yamelenga kutoa elimu ya miliki bunifu mashuleni na kukuza vipaji vya ubunifu kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari.
Kitaifa mashindano hayo yalihusisha Shule tano ambazo zilikuwa ni Shule ya Ufundi Tanga, Shule ya Sekondari Sikirari, Shule ya Sekondari Kiembe Samaki - Zanzibar, St. Joseph Sekondari na Makongo Sekondari waliibuka washindi kitaifa.
Kimataifa mashindano hayo yamehusisha Wanafunzi kutoka nchi tano za Afrika ikiwemo Gambia,Ghana,Zambia,Liberia na Rwanda.
