Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, akigawa Tuzo pamoja na Vyeti kwa Mikoa iliyofanya vizuri katika Mashindano ya Ngoma na Vyakula vya Asili tarehe 29 Agosti wakati akihitimisha Tamasha la Utamaduni la Kitaifa mkoani Morogoro.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA Bi. Naomi Mungure (kushoto) akimkabidhi leseni iliyohuishwa Meneja Leseni Kampuni ya Society of Music Advocacy (SOMA) Bw. Davis Kalokola kwa ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha ya kazi za Muziki tarehe 27 Julai, 2026.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA Bi. Naomi Mungure (kulia) akimkabidi leseni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Audio Visual (TAVIC) Bw. Jesse Madauda ya ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha ya kazi za vielelezo vya kusikia na kuona (Audiovisual) tarehe 27 Julai, 2026.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA Bi. Naomi Mungure (kushoto) akimkabidhi leseni iliyohuishwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Reproduction Rights Society Limited (TANRRS) Bw. Abdallah Saiwad kwa ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha ya kazi za maandishi (literary works) tarehe 27 Julai, 2026.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akimwapisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda (Mb) Leo tarehe 13 Januari, 2026 katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Hamis Mwinjuma kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Novemba 18, 2025 Ikulu jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndg. Methuthela Stephen Ntonda kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti, 2024.
Meneja Usajili na Kumbukumbu kutoka Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bw. Philemon Kilaka akitoa mafunzo ya hakimiliki na umuhimu wa usajili wa kazi za Sanaa na Uandishi kwa Wasanii na Waandishi wa vitabu wa Songea Mjini leo tarehe 27.04.2024. katika semina ya mafunzo kwa wadau hao iliyoandaliwa na taasisi zilizochini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo zinazosimamia kazi za Sanaa nchini.
Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Miliki Bunifu la Kikanda la Afrika (ARIPO) Amadu Bah (kulia) akikanidhi hundi ya mfano ya mgao wa mirabaha wa msanii Raymond Mwakyusa (Rayvanny) iliyopokelewa kwa niaba yake na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na mdau wa muziki Mhe. Shaban Hamis Taletale, katika hafla ya mgao wa mirabaha, Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Bima TIRA Dkt. Baghayo Saqwera (kushoto) akikabidhi hundi ya mfano ya mgao wa mirabaha wa msanii Nasibu Abdul (Diamondplatinumz) iliyopokelewa kwa niaba yake na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na Mdau wa muziki Mhe. Shaban Hamis Taletale, katika hafla ya mgao wa mirabaha, Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.